KIKOSI CHA SIMBA SC KIMEWASILI SALAMA DUBAI TAYARI KWENDA MORROCO

Kikosi kimefika salama Dubai. Safari itaendelea saa 1:45 asubuhi kuelekea Casablanca kwa kupitia Tunis.

Pichani ni Kundi la Wachezaji wa Simba SC 

Katika michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika ( CAF CHAMPIONS LEAGUE) imeweka Historia Kwa mara ya kwanza kutinga Robo fainali ukiachia michuano iliyopita kuishia hatua ya Makundi. 

Simba SC  kabla ya kuingia Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepoteza Michezo miwili Wakiwa ugenini. Mechi ya Kwanza walipoteza Mbele ya HOROYA AC kwa kufungwa 1-0. 

Mechi nyingine walipoteza Mbele ya RAJA CASABLANCA kwa kufungwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa 3-0. 

Mechi walizoshinda Simba SC ni kwa kuwafunga VIPERS FOOTBALL CLUB pamoja na HOROYA kabla ya kutinga Hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika #CAFCL. 

Mechi ijayo Simba SC anaenda Ugenini Kucheza na WYDAD CASABLANCA katika uwanja wa MOHAMMED 5 baada ya Kupata Ushindi wa Goli moja kwa sifuri 1-0 katika Uwanja wa Mkapa. 

#SimbaSC #CAFCL #ligiyamabingwaafrika #CAFChampionsLeague #wydadCasablanca #SimbaWydadCasablanca #wydadCasablancaVsSimbaSC#nguvumoja #mutramastory255.blogspot.com 



Comments